Taarifa iliyotolewa na idara hiyo inasema kuwa licha ya kuwa Msikiti Mkuu wa Paris ni sehemu mashuhuri ya ibada kwa Waislamu lakini wakati huohuo ni sehemu ya kuvutia watalii na nembo ya kukumbukwa askari wa Kiislamu wa Ufaransa waliopigania nchi hiyo wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Imeendelea kusema kuwa msikiti huo pia ni nembo ya urafiki wa Uislamu na Ufaransa.
Maafisa wa posta ya Ufaransa wamesema stempu hiyo itazinduliwa tarehe 11 Februari na kusambazwa katika idara zote za posta nchini tarehe 13 mwezi huohuo.
Msikiti Mkuu wa Paris ndio msikiti mkubwa zaidi nchini Ufaransa na wa tatu kwa ukubwa barani Ulaya. Msikiti huo ulio na mnara wenye urefu wa mita 33 ulijengwa mwaka 1922 kama alama ya kuwashukuru askari wa Kiislamu waliopigana katika Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia kulinda ardhi ya Ufaransa.
Askari laki moja kati ya hao walipoteza maisha yao katika vita hivyo dhidi ya Ujerumani. 928888