Uamuzi huo umekuja baada ya Waislamu Uganda kulalamikia uamuzi wa awali wa uongozi wawa chuo hicho kumzuia mwanamke Muislamu kuingia katika ukumbi wa mitihani akiwa amevaa hijabu. Mwanafunzi huyo mwenye kutii mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu alifadhilisha kukosa mitihani kuliko kumuasi Mwenyezi Mungu
Waislamu wakiongozwa na Sheikh Nuhu Muzata wamesema Chuo Kikuu cha Makerere kinapaswa kubadilisha sheria zake za mitihani ili kuwaruhusu wanafunzi wa kike.
Sheikh Mutaza amesema kuwa tatizo kubwa ni kuwa hakuna mwakilishi wa Waislamu katika Baraza la Chuo Kikuu cha Makerere na hivyo kupelekea masuala muhimu ya Waislamu kupuuzwa.
Uganda ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ni nchi yenye idadi kubwa ya Waislamu. Mwamko wa Kiislamu unashuhudiwa katika maeneo yote ya dunia ambapo Waislamu wanasisitiza kutekeleza mafundisho na maamurisho ya dini yao.
928545