Kwa mujibu wa tovuti ya ISESCO, kitabu hicho kimeandikwa na Dr. Shawqi Shaat mkurugenzi wa zamani wa majumba ya makumbusho kaskazini mwa Syria.
Katika dibaji ya kitabu hicho chenye kurasa 304, Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO, Dr. Abdulazizi Othman Altuwaijri ameashiria azma ya ISESCO ya kuimarisha mikakati ya utamaduni hasa kuboresha majumba ya makumbusho na kulinda hifadhi za kiakiolojia na kisanaa za nchi wanachama wa OIC.
Amesema ISESCO inazingatia kwa kina suala la kulinda turathi za nchi za Kiislamu kwani ni sehemu muhimu ya ustaarabu. Aidha amesema ISESCO ina mpango wa kutoa mafunzo kwa wataalamu kuhusu kulinda turathi za Kiislamu mbali na kuhakikisha kuwa teknolojia za kisasa zinatumika katika taaluma hiyo.
928854