Imesisitiza kwamba bivaraka hao ni vyombo vyenye thamani ndogo vinavyotumiwa na Marekani dhidi ya Waislamu. Hizbullah imesema kuwa milipuko hiyo ni ukurasa mpya wa mipango ya kulipiza kisasi inayotekelezwa na Marekani dhidi ya taifa la Iraq ili kufunika fedheha ya kushindwa na kulazimika kuondoka kwake katika ardhi ya nchi hiyo.
Hizbullah imesisitiza katika sehemu ya taarifa yake kwamba magaidi wametekeleza milipuko hiyo ya kinyama, ambapo baadhi imewalenga wafanyaziara wa maeneo matakatifu, kwa lengo la kuzusha fitina, unafiki na hitilafu nchini Iraq ili kudhamini maslahi ya wageni nchini humo.
Taarifa ya Hizbullah imeyataka makundi yote ya kisiasa ya Iraq kuzima njama hizo hatari za Marekani na kuimarisha umoja miongoni mwao. Huku ikiomboleza na familia za mashahidi wa milipuko hiyo ya kigaidi Hizbullah imewaombea shifaa na nafuu ya haraka wale wote waliojeruhiwa katika milipuko hiyo. Zaidi ya watu 67 waliuawa na wengine 138 kujeruhiwa katika milipuko hiyo. 929828