IQNA

Kushambuliwa maeneo ya Kiislamu ni jinai dhidi ya ubinadamu

14:48 - January 08, 2012
Habari ID: 2252979
Taasisi ya Uhusiano wa Kitaifa ya Canada FCRR imeitaka polisi ya nchi hiyo kuyatambua mashambulio yanayofanywa dhidi ya maeneo ya Kiislamu kuwa ni jinai dhidi ya ubinadamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya newswire, taasisi ya FCRR imetoa taarifa ikilaani vikali shambulio la hivi karibuni lililofanywa na kundi la watu wenye misimamo ya kupindukia mipaka katika misikiti na maeneo ya ibada ya Kiislamu nchini humo na kuitaka polisi kuyatambua mashambulio kama hayo kuwa ni jinai dhidi ya ubinadamu.
Sehemu moja ya taarifa hiyo inasema kuwa taasisi ya FCRR ina wasiwasi mkubwa kuhusiana na kuongezeka vitendo vilivyo dhidi ya Uislamu na mashambulio katika maeneo ya kidini na kuongeza kuwa mashambulio hayo yanaonyesha wazi ongezeko la vitendo vya mabavu na chuki dhidi ya jamii ya Waislamu nchini humo.
Taarifa ya FCRR imesema jamii ya Canada haikubali suala hilo. Sehemu ya mwisho ya taarifa hiyo inasema kwamba taasisi ya FCRR itashirikiana na taasisi pamoja na mashirika mengine ya kitaifa na kimataifa kwa madhumuni ya kuimarisha mazungumzo ya kidini na kiutamaduni kwa lengo la kuimarisha umoja na kupambana na vitendo vilivyo dhidi ya thamani za kidini nchini humo. 930792
captcha