IQNA

Watawala wa Bahrain wabomoa misikiti 20

13:29 - January 10, 2012
Habari ID: 2254524
Mkuu wa kamati ya chama cha al Wifaq al Islami kilichojiuzulu kutoka Bunge la Bahrain amesema kuwa watawala wa Aal Khalifa wameharibu kwa makusudi misiki 20 ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa televisheni ya al-Alam, hayo yamesemwa na Abdul Jalil Khalil mkuu wa kamati hiyo iliyojiondoa katika Bunge la Bahrain na kuongeza kuwa hatua hiyo ilitekelezwa na watawala hao kinyume cha sheria.
Ameendelea kusema kuwa watawala hao wamekuwa wakizuia na kuvuruga juhudi za kujengwa msikiti mkubwa zaidi nchini humo bila kutoa sababu zozote zinazokubalika. Mbunge huyo aliyejiuzulu amesema kwamba tokea mwaka 1974 watawala wa Bahrain wamekuwa wakikataa kusajili taasisi na jumuiya yoyote ya wakfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Khalil pia ameutaka utawala wa Bahrain kukarabati na kujenga upya misikiti yote uliyoiharibu, kuwafikisha mahakamani wahusika wote wa uharibifu huo wa maeneo ya ibada na kusajili wakfu za Mashia ambao wanaunda idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo. 932191
captcha