IQNA

ٌWarsha ya Uislamu na Vyombo vya Habari yafanyika Malawi

20:48 - January 10, 2012
Habari ID: 2255032
Warsha ya mafunzo ya Uislamu na Vyombo vya Habari imefanyika katika mji wa Limbe nchini Malawi ikihudhuriwa na waandishi habari wasiokuwa Waislamu.
Afisa wa Jumuiya ya Habari ya Kiisalmu ya Malawi Dinala Chabolika amesisitiza katika warsha hiyo juu ya udharura wa waandishi habari kuakisi ukweli wa mambo kuhusu dini ya Uislamu ili kuzuia wimbi la kuwapotosha wananchi.
Ameashiria baadhi ya maneno yanayotumiwa vibaya na sura isiyokuwa sahihi inayotolewa na vyombo vya habari kuhusu dini ya Uislamu na kuwatahadharisha waandishi habari juu ya kuandika habari zisizokuwa za kweli kuhusu dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Chabolika amesema, miongoni mwa masuala yanayoakisiwa visivyo kuhusu Uislamu ni nafasi ya mwanamke katika dini hiyo. Amesema kuwa mwanamke katika Uislamu amepewa heshima kubwa na haki nyingi katika nafasi zake zote kama mke, mama au dada. 932991
captcha