Kufuatia kifo cha msomi huyo ambaye pia alikuwa mwanachama wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as), Hujjatul Islam wal Muslimin Abbas Ali Akhtari, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo ametuma salamu za rambirambi ambapo ameomboleza kifo cha msomi huyo aliyemtaja kuwa mwanafikra na mtafiti muhimu. Amesema msomi na mtarjumi huyo alitumia umri wake wenye mbaraka kueneza maarifa na ujumbe wa Ahlul Bait (as) katika jamii iliyo na utamaduni na ustaarabu mkongwe ya Japan.
Sheikh Akhtari amesema maisha yake matukufu yalijaa mafundisho ya takwa na uchaji-Mungu kwa jamii hiyo. Amesema bila shaka vitabu vingi alivyoandika na wanafunzi wema aliolea watakuwa na nafasi muhimu katika kuhuisha jina lake miongoni mwa waja wema katika historia ya Kiislamu na Kishia.
Mwishoni mwa ujumbe huo wa rambirambi Hujjatul Islam Akhtari amewatakia subira Waislamu wa Japan, familia na hasa mwanawe wa kiume Hujjatul Islam wal Muslimin Ibrahim Tatasoichi Sawada, katika kipindi hiki kigumu na kumwombea maghfira marehemu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Tatasoichi Sawada kwa sasa ndiye mkurugenzi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as) mjini Tokyo Japan. Amekuwa na nafasi muhimu katika kueneza maarifa ya Qur'ani na ya Ahlul Beit (as) nchini humo. 933313