IQNA

Sheikh wa al al Azhar:

Niko tayari kwenda Palestina na kufa shahidi

18:49 - January 11, 2012
Habari ID: 2255731
Sheikh wa al Azhar nchini Misri Ahmad Tayyib amesema kuwa yuko tayari kwenda Palestina kwa ajili ya kupigana na kufa shahidi iwapo makundi ya Kipalestina yataungana na kuwa na umoja.
Sheikh wa al Azhar amesema mapambano ya ukombozi ni haki ya kisheria ya Wapalestina inayokubaliwa na sheria za Kiislamu na kanuni za kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na Sheikh wa al Azhar imesema: Mapambano ya wananchi wa Palestina dhidi ya maghasibu wa utawala wa Kizayuni ni haki yao ya wazi inayotambuliwa rasmi na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Amesisitiza kuwa yuko tayari kwenda Palestina na kufa shahidi katika ardhi ya nchi hiyo iwapo makundi na vyama vya Palestina vitaungana.
Sheikh Tayyib amesema, jihadi na mapambano dhidi ya adui ni jambo la dharura kwa sababu Wazayuni hawawezi kuondoka katika ardhi ya Palestina bila ya kulazimishwa. 933293
captcha