IQNA

Kitendo cha kumuua shahidi msomi wa Iran ni ishara ya chuki ya maadui

11:26 - January 12, 2012
Habari ID: 2255778
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran amelaani vikali kitendo cha kigaidi cha mabeberu wenye upofu wa moyo cha kumuua shahidi msomi wa Kiirani Bw. Mustafa Ahmadi Roshan na kusema kuwa, kitendo hicho cha kigaidi kinathibitisha jinsi maadui walivyo na chuki kubwa dhidi ya taifa la Iran.

Dk. Ali Larijani ametoa ujumbe maalumu kuhusu suala hilo akisema: Kwa mara nyingine maadui wajinga, masafihi na majahili wamemuua shahidi msomi na mhadhiri wa Chuo Kikuu wa Iran Dk. Mustafa Ahmadi Roshan na hii si mara ya kwanza kwa mabeberu wapofu wa nyoyo kufanya kitendo kama hicho cha kigaidi lakini ugaidi wao huo hauwezi kukwamisha nia thabiti mithili ya chuma ya taifa la Iran na mwamko wa taifa hili wa kusimama imara katika misimamo yake.
Pia amesema, shahid Mustafa Ahmadi Roshan alikuwa mmoja wa wahadhiri wanaohudumia vilivyo masuala ya kielimu nchini na kuuliwa kwake shahidi na maadui kunaonesha ni jinsi gani maadui hao walivyo na chuki kubwa na wananchi wa Iran.
933525
captcha