IQNA

Kimya cha nchi za Kiislamu mbele ya Wazayuni ni kosa kubwa

19:05 - January 12, 2012
Habari ID: 2255867
Kimya cha baadhi ya nchi muhimu katika Ulimwengu wa Kiislamu mbele ya jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina ni kosa kubwa la kistratijia, amesema mtaalamu mmoja wa kisiasa nchini Iran.
Katika mahojiano na IQNA, Katibu Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha Iran Abulqasim Raufian amesema pamoja na kuwa serikali za nchi za Kiislamu zimelala lakini wananchi wameamka.
Ameashiria uamuzi wa bunge la utawala haramu wa Israel, Knesset, kutangaza Quds kama mjii mkuu wa utawala huo na kusema sera hiyo inalenga kuwatia motisha wale Wazayuni walioshawishiwa na utawala huo kuhamia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Amesema Wazayuni hao sasa wameingiwa na kiwewe kufuatia mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Amesema kuwa uamuzi huo wa bunge la Kizayuni ni ishara ya wasiwasi wao mkubwa kuhusu siku za usoni.
Akijibu swali kuhusu chanzo cha kimya cha baadhi ya nchi za Kiislamu kuhusu uamuzi wa kichokozi wa Knesset, Raufian amesema nchi hizo ni vibaraka wa utawala wa Kizayuni na madola ya Kimagharibi hasa Marekani na hivyo zinaogopa kusimama kidete dhidi ya sera za kujitanua mbele ya utawala haramu wa Israel.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hatua ya bunge la utawala wa Kizayuni ya kutangaza Quds Tukufu kuwa mji mkuu wake. Iran imetoa wito kwa nchi zote za Kiislamu na mataifa yote yapendayo uhuru duniani kuchukua hatua za kivitendo dhidi ya uchokozi huo wa Israel.
931000
captcha