IQNA

Uswisi yakwamisha shughuli za Baraza Kuu Waislamu

11:59 - January 15, 2012
Habari ID: 2256849
Viongozi wa mji wa Buelach nchini Uswisi wamefuta kongamano la kimataifa la 'Umoja wa Kiislamu' lililokuwa limepangwa kufanyika katika mji huo.
Taarifa iliyotolewa na Baraza Kuu la Waislamu wa Uiswisi imesema kuwa, maafisa wa mji wa Buelach wamefuta makubaliano yao na taasisi hiyo ya Kiislamu ya kukodisha ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kungamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu mwaka 2012.
Taarifa hiyo imesema kuwa, maafisa wa mji huo wanataka kuzuia kongamano hilo kwa kisingizio kwamba Baraza Kuu la Waislamu la Uswisi ni taasisi yenye misimamo ya kufurutu ada!
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa maafisa wa mji wa Buelach walikuwa tayari wametia saini mkataba wa kulikodisha Baraza Kuu la Waislamu ukumbi wa mikutano wa mji huo na uamuzi wao wa sasa unaonesha kuwa kuna njama inayofanywa na viongozi hao dhidi ya Waislamu.
Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu mwaka 2012 limepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao wa Februari chini ya usimamizi wa Baraza Kuu la Waislamu wa Uswisi na litahudhuriwa na wasomi na wanafikra kuitoka nchi mbalimbali duniani. 934334
captcha