Akizungumza hivi karibuni na mashirika ya habari nchini Lebanon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kulengwa raia wa kawaida na wasomi kupitia vitendo vya kigaidi ni jambo lisilokubalika kabisa na kwamba linapasa kulaani kwa kila njia.
Amesema Lebanon ni nchi muhimu iliyo na athari kubwa katika matukio ya Mashariki ya Kati na vilevile katika kuleta amani na utulivu katika eneo hili. Ameongeza kuwa Lebanon ina nafasi muhimu mbele ya jamii ya kimatifa na hasa Umoja wa Mataifa katika kuimarisha utulivu Mashariki ya Kati na ndio maana akaichagua kuwa kituo cha kwanza cha safari yake katika eneo hili.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria matukio ya Syria na kusema kuwa anaunga mkono mpango wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu kwa ajili ya kutatuliwa mgogoro huo. 934871