Msahafu huo utakuwa sehemu ya maonyesho yenye anwani ya, “Hija, Safari Katika Moyo ya Uislamu”. Maonyesho hayo yatakuwa ni mjumuiko wa kwanza kabisa maalumu kwa ajili ya Hijja.
Kwa mujibu wa Jumba la Makumbusho la Uingereza, inasadikiwa kuwa Msahafu huo ni wa karne ya 8 Miladia. Ushahidi uliopo unaoyesha kuwa, yamkini uliandikwa Makka au Madina na ni kati ya misahafu iliyoandikwa mapema katika historia ya Uislamu.
Msahafu huu sawa na misahafu mingi ya kale hauna ‘harakati’. Mtaalamu mwandamizi wa Jumba la Makumbusho la Uingereza David Jacobs ameliambia gazeti la Arab News kuwa: “Nuskha hii ya Qur’ani ilimilikiwa na Jumba la Makumbusho la Uingereza karne ya 19”.
Amesema kutokana na ugumu wa kuuhifadhi msahafu huo, ni nadra sana kuonyeshwa hadharani kwa muda mrefu.
Maonyesho hayo ya Hija yameandaliwa kwa ushirikiano na Maktaba ya Umma ya Mfalme Abdulaziz.
934980