IQNA

Msahafu mkubwa zaidi ulioandikwa kwa mkono

11:56 - January 15, 2012
Habari ID: 2256969
Msahafu mkubwa zaidi ulioandikwa kwa mkono umezinduliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa kidini na kiserikali mjini Kabul, Alkhamisi iliyopita.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mradi huo ulipendekezwa na Alhaj Sayyid Mansoor Naderi.
Uandishi wa msahafu huo mkubwa zaidi duniani ulichukua kipini cha miaka mitano kukamilishwa na jopo la wataalamu chini ya usimamizi wa Hakim Nasir Khusrow Balkhi.
Kazi hiyo yenye thamani ilianza Septemba mwaka 2004 na ilimalizika Septemba mwaka 2009. Kazi ya kaligrafia imefanyika katika kurasa 218 ambapo ina nakala hiyo ya Qur'ani upana wa centimita 228 na upana wa centimita 155.
Juzuu zote 30 za Qur’ani Tukufu zimeandikwa kwa miundo 30 tafauti.
Akizungumza katika hafla hiyo Sayyid Mansoor Naderi amesema kumalizika msahafu huo ni mafanikio makubwa kwa taifa la Afghanistan na nchi zote za Kiislamu duniani.
935007
captcha