IQNA

2012: ‘Mwaka wa Qur’ani Tukufu’ Tatarstan

14:31 - January 15, 2012
Habari ID: 2256985
Jamhuri ya Tatarstan katika Shirikisho la Russia imetangaza mwaka 2012 kuwa ‘Mwaka wa Qur’ani Tukufu.
Hayo ni kwa mujibu wa taangazao la Taasisi Kuratibu Masuala ya Waislamu katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, uamuzi huo umechukuliwa kwa mujibu wa mpango wa Taasisi ya Kuratibu Masuala ya Waislamu wa kuandaa programu kadhaa za sayansi za Qur’ani na kuhakikisha kuwa Waislamu wa eneo hilo wanaifahamu vizuri Qur’ani Tukufu.
Aidha Uldüz Hazrat Feizov Mufti wa Tatarstan ambaye ndio mkuu wa Taasisi ya Kuratibu Masuala ya Waislamu ameashiria umuhimu wa kutangazwa mwaka 2012 kuwa mwaka wa Qur’ani Tukufu na kuongeza kuwa taasisi hiyo pamoja na wanazuoni nchini humo wanapanga harakati kadhaa za Qur’ani mwaka huu.
Kwa mujibu wa Sheikh Mohammad Shinn, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Russia amesema mipango ya Qur’ani iliyopangwa ni pamoja na mashindano ya Qur’ani na maonyesho ya Sanaa za Kiislamu.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa iko tayari kuandaa maonyesho kadhaa ya kaligrafia pamoja na maonyesho kadhaa ya Qur’ani.
Jamhuri ya Tatarstan ambayo mji wake mkuu ni Kazan ni sehemu ya Shirikisho la Russia na iko katika Jimbo la Volga.
933543
captcha