IQNA

Msikiti mkubwa zaidi nchini Uswisi kujengwa

14:53 - January 16, 2012
Habari ID: 2257704
Baraza Kuu la Waislamu wa Uswisi limetangaza azma yake ya kujenga msikiti mkubwa zaidi nchini humo katika mji wa Bern.
Kwa mujibu wa tovuti ya tdg, vyombo vya habari vya Uswisi vimetangaza kwamba baraza hilo linafanya mazungumzo na viongozi wa kidini wa nchi za Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kutayarisha bajeti ya ujenzi wa msikiti huo katika mji mkuu wa Uswisi.
Baraza hilo limesema kwamba franca milioni 20 za Uswisi zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo na kwamba mazungumzo ya kuandaa bajeti hiyo yangali yanaendelea. Limesema mazungumzo ya kupata wafadhili yanahitaji muda mrefu na kwamba linafuatilia wafadhili ambao licha ya kuwekeza katika mradi huo muhimu wataweza kuandaa mazingira mazuri ya kuimarisha ushirikiano wa kiutamaduni kati ya Waislamu wa Uswisi na Waislamu wa nchi nyinginezo za ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Nicolas Blancho Mkuu wa Baraza la Waislamu wa Uswisi mwaka uliopita alisafiri nchini Kuwait ambapo alionana na kuzungumza na viongozi wa serikali pamoja na wafanyabiashara wakubwa wa nchi hiyo na kujadiliana nao kuhusu ujenzi na ufadhili wa msikiti huo. 935654
captcha