IQNA

Umoja wa Mataifa walaani ujenzi wa vitongoji vya Mayahudi

14:57 - January 16, 2012
Habari ID: 2257909
Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa jana Jumapili aliwataka wakuu wa utawala haramu wa Israel wasimamishe mara moja ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina unazozikalia kwa mabavu.
Kwa mujibu wa gazeti la Le Figaro la Ufaransa Ki-Moon alitoa tahadhari ya kusimamishwa ujenzi wa vitongoji hivyo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari huko Beirut mji mkuu wa Lebanon. Amesema ujenzi wa vitongoji hivyo unapasa kusimama mara moja kwa sababu unazuia kuundwa kwa nchi huru ya Palestina.
Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, Ban Ki-moon amesema kuwa vitongoji vyote vya zamani na vya sasa ni haramu na kwamba vinapaswa kusimamishwa.
Vilevile amelaani vitendo vya mabavu na mashambulio yanayofanywa na askari wa utawala haramu wa Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina na kusisitiza kuwa jambo hilo haliwezi kuvumiliwa wala kukubalika. Amesema tayari Umoja wa Mataifa umewaonya watawala wa Tel Aviv kuhusiana suala hilo. 936011
captcha