Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kituo hicho kitazingatia masuala ya sheria za Kiislamu na maadili na kinasimamiwa na Sheikha Moza bint Nasser, Mwenyekiti wa Waqfu wa Qatar wa Elimu, Sayansi na Ustawi wa Jamii.
Sherehe za kuzinduliwa kituo hicho zilizofanyika siku ya Jumapili zikihudhuriwa na wasomi mbalimbali akiwemo Sheikh Yusuf Qaradawi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu.
Akizungumza katika halfa hiyo, Sheikha Moza amesema: 'Naamini kuwa kwa kuzingatia maendeleo ya milenia iliyopita, kuna haja ya kubuni taasisi ya utafiti yenye uwezo wa kufanya utafiti mpana kuhusu fikra za Kiislamu.
Sheikha Moza amesema ujumbe wa taasisi hiyo unapaswa kuwa katika misingi ya kimataifa na hivyo kulea watu ambao wataleta mabadiliko katika jamii.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Sheria na Maadili ya Kiislamu ni Dr. Tariq Ramadhan, msomi mashuhuri wa Kiislamu barani Ulaya.
935867