IQNA

Waislamu Australia wataka historia yao ilindwe

17:01 - January 17, 2012
Habari ID: 2258182
Waislamu nchini Australia wamewasilisha ombi la kutaka kujengwa jengo la makumbusho litakaloonyesha turathi yao nchini humo.
Kwa mujibu wa The Sunday Canberra Times, Shirikisho la Mabaraza ya Kiislamu Australia limesema katika ombi lake hilo kuwa: 'Mchango wa Waislamu katika ustawi wa Australia ni sehemu ya turathi ya Waustralia wote, kwa hivyo tunaomba kupewa kipande cha ardhi mjini Canberra'.
Waislamu waliwasilisha ombi lao hilo Aprili 2011 na wanakusudia kujenga 'Jengo la Makumbusho la Historia na Sanaa ya Kiislamu'.
Akiwasilisha ombi hilo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Mabaraza ya Kiislamu Australia amesema jengo hilo la makumbusho litakuwa na mchango mkubwa katika mji wa Canberra na litawaelimisha Waustralia kuhusu turathi ya Waislamu huko Australia katika kipindi cha karne mbili zilizopita.
935860
captcha