Kwa mujibu gazeti la Al Yawm Al Sabe kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Misri kwa ushirikiano na wanazuoni kadhaa wa Hadithi chini ya usimamizi wa Sheikhe Mkuu wa Al Azhar, Sheikh Ahmad Tayyeb.
Kati ya malengo ya kongamano hilo ni kuimarisha uhusiano wa wanazuoni wa Hadith na kuwawezesha kubadilisha mawazo kuhusu taaluma ya sayansi za Hadithi.
Washiriki wamejadili suala la sanadi za hadithi na umuhimu wa kukusanya nyaraka za kale katika utafiti. Aidha wamejadili masuala ya teknoloajia na Suna.
Kati ya walioshiriki katika kikao hicho ni wanazuoni wa Hadithi kutoka Chuo Kikuu cha Al Azhar, Chuo Kikuu cha Cairo na vilevile vyuo vikuu vya Morocco, Algeria, Tunisia, Saudi Arabia, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Kuwait, Syria, Lebanon, India, Bahrain na Jordan.
Kati ya waliohudhuria ni Sheikh Ali Gomaa, Mufti of Misri na wanazuoni wa hadithi katika Ulimwengu wa Kiislamu kama vile Mohammad ‘Awamah, Bashshar Awad Ma’ruf, Ahmad Umar Hashem, Ahmad Mohammad Noor Seyf, Nuruddin Atar, Raf’at Fowzi Abdul Mottaleb, Mostafa Mohammad Abu Amarah, Abdul Majid Mahmoud Abdul Majid na Marwan Mohammad Mostafa.
935314