IQNA

Kikao cha Haki za Binadamu katika Uislamu chafanyika Uganda

15:45 - January 18, 2012
Habari ID: 2259100
Kongamano la Haki za Binadamu katika Uislamu limefanyika nchini Uganda huku kukitolewa wito wa kuishi kwa amani na maelewano kwa mujibu wa Suna za Mtume SAW.
Mkuu wa Kituo cha Waislamu cha Uadilifu na Sheria cha Uganda Jaffer Senganda amesema semina hiyo ya siku tatu inayomalizika leo inakusudia kurekebisha taswira potofu ya maadui wanaodai kuwa Uislamu unaenezwa kwa mabavu.
Ameongeza kuwa semina hiyo inategemea mafundisho ya Qur'ani katika kuoneysha kuwa Uislamu ni dini ya amani. Amesema kutoa mafunzo ya haki za binadamu miongoni mwa Waislamu ni jambo muhimu ili kuepusha migogoro katika jamii.
Naye Sheikh Badru Byamugisha ametoa wito kwa washiriki katika semina hiyo kutoiga jinai zinazotekelezwa na makundi kama Boko Haram dhidi ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu nchini Nigeria. Amesema harakati za kundi la Boko Haram zinaenda kinyuma cha mafundisho ya Kiislamu.
936684
captcha