Kundi moja la intaneti la wanaharakati wa Kiislamu lijulikanalo kama CPI limesema kufuatia hatua ya utawala haramu wa Israel kutangaza Quds kama mji mkuu wa Wazayuni, kampeni ya 'Quds Mji Mkuu wa Umma wa Kiislamu' imeanzishwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
'Kamati ya Maandamano ya Kurejea Palestina' ni kati ya makundi yaliyoanzisha kampeni hiyo.
Taarifa ya kamati hiyo imesema kuwa, sambamba na kushadidi hujuma za Wazayuni dhidi ya maeneo matakatifu ya Kiislamu katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu pamoja na njama za kuuyahudisha mji wa Quds, Waislamu wote duniani wanapaswa kuungana katika kulinda matukufu ya Kiislamu huko Palestina.
Hivi karibuni bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Knesset, liliidhinisha mpango wa kutangaza Quds Tukufu kuwa mji mkuu wa utawala huo na taifa la Mayahudi.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa wito kwa nchi za Kiislamu kuchukua hatua za haraka na za pamoja kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuufanya mji wa Baitul Muqaddas kuwa na sura ya Kiyahudi.
937304