Picha hizo zilizoonyeshwa kwenye televisheni ya serikali zinamuonesha mtu huyo akiandika maandishi machafu dhidi ya Waislamu na kujaribu kuchoma msikiti na kituo cha Kiislamu cha mji huo.
Kuhusu sababu za kuonyeshwa picha hiyo, polisi ya Canada imetangaza kuwa picha hizo zilinaswa na kamera za usalama za Kituo cha Waislamu lakini hadi sasa polisi imeshindwa kumtia nguvuni mhalifu huyo; kwa msingi huo polisi imeamua kuonesha picha zake kwa shabaha ya kupata ushirikiano wa wananchi katika suala hilo.
Taarifa ya polisi ya Canada imesema kuna matumaini kwamba mhalifu huyo atatiwa nguvuni kwa msaada wa wananchi. Imewataka pia wananchi kuripoti polisi iwapo watamuona mhalifu huyo.
937324