Mashindano hayo yatasimamiwa na Kituo cha Hifdhi ya Qur’ani cha Abu Dhabi na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu na Wakfu la Imarati. Mashindano hayo yanajumuisha hifdhi ya juzuu 20, 15, 10, 5, 3 na juzu 2.
Wasimamizi wa mashindano hayo wametayarisha pia mashindano makhsusi kwa watu wenye maradhi makhsusi, mashindano ya tajwidi bora na mashindano ya Taajul Wiqar kwa ajili ya familia.
Ratiba nyingine ya mashindano hayo ni pamoja na kuwaenzi wahudumu mashuhuri wa Qur’ani ambapo mwaka jana wasomaji bora wanne wa kiume na wanne wa kike walienziwa.
Washindi wa duru ya tatu ya mashindano ya hifdhi ya Qur’ani ya Khalifa bin Jabir watatunukiwa zawadi katika sherehe itakayohudhuriwa na wasimamizi wa mashindano hayo. 938259