IQNA

Mashindano ya Qur'ani Sudan kufanyika kila mwaka

14:57 - January 23, 2012
Habari ID: 2261380
Rais Omar al Bashir wa Sudan amesema kuwa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Sudan yatafanyika kila mwaka nchini humo.
Akizungumza mjini Khartoum katika sherehe za kufunga Duru ya Pili ya Mashindano ya Kimataifa ya 'Zawadi ya Qur'ani ya Khartoum' Januari 22, Rais Bashir amewataka watawala wa majimbo ya Sudan kuongeza juhudi zao za kuunga mkono harakati za Qur'ani. Rais Bashir amesema atafanya kila awezalo kuunga mkono shughuli za Qur'ani.
Rais Bashir ameongeza kuwa: 'Qur'ani ndio sheria na kanuni yetu na sisi Wasudani kwa kufungamana na Qur'ani tutajilinda na njama za maadui'.
Ameongeza kuwa: 'Historia ya Sudan inafungamana na Qur'ani Tukufu na Wasudani wangali wanafungamana na Qur'ani na wamechukua hatua katika kutekeleza Wahyi na Sira ya Mtume SAW'.
Huko nyuma Mashindano ya Kimataifa ya 'Zawadi ya Qur'ani ya Khartoum' yalikuwa yakifanyika kila miaka miwili lakini sasa yatakuwa yakifanyika kila mwaka.
Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na washiriki 250 wakiwemo maqari na mahufadhi kutoka zaidi ya nchi 30 duniani ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Iraq, Syria, Kuwait, Saudi Arabia, Uturuki, Misri, Libya, Qatar, Ethiopia, Afrika Kusini, Chad na Senegal.
939610
captcha