IQNA

OIC yalaani kutiwa mbaroni spika wa Bunge la Palestina

15:10 - January 23, 2012
Habari ID: 2261409
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiisilamu (OIC) imelaani hatua za utawala wa Israel ya kumtia mbaroni Spika wa Bunge la Palestina.
Ekmeleddin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiisilamu (OIC) amelani hatua ya Wazayuni ya kumtia mbaroni Spika wa Bunge la Palestina Aziz Duwaik na amesema, bila shaka hatua hiyo inadhihirisha jinsi Wazayuni wanavyozipa kisogo sheria za kimataifa na kwamba, hatua hiyo ni njama chafu dhidi ya Wapalestina.
Ihsanoglu amesistiza ulazima wa kuachiwa haraka Aziz Duwaik kutoka katika magereza ya Wazayuni. Katibu mkuu wa OIC pia ameyataka mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yalaani hatua hiyo ya Israel.
Aziz Duwaik alikamatwa tarehe 19 mwezi huu katika kituo kimoja cha ukaguzi huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kabla ya hapo aliwahi kukamatwa na utawala huo ghasibu na kubakia katika gerezani kwa miezi 36.
Wabunge 25 wa Palestina 21 kati yao wakiwa ni wa Harakati ya Muqawama wa Palestina Hamas wanashikiliwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
939114
captcha