IQNA

Kongamano la Mwamko wa Kiislamu wa Kimataifa kufanyika Uingereza

17:31 - January 23, 2012
Habari ID: 2261546
Kongamano la Mwamko wa Kiislamu wa Kimataifa litafanyika tarehe 12 Februari katika Kituo cha Kiislamu cha Uingereza mjini London.
Kongamano hilo litafanyika sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Kiislamu kwa hima ya Kituo cha Kiislamu cha Uingereza na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as) tawi la London.
Kongamano hilo litahutubiwa na wasomi, shakhsia na wanasiasa kutoka nchi mbalimbali.
Maudhui kuu ya kongamano hilo ni Mwamko wa Kiislamu na taathira zake katika matukio ya Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika. 939557


captcha