IQNA

Mashia wa Misri wakumbuka siku ya kufariki dunia Mtume (saw)

17:30 - January 23, 2012
Habari ID: 2261548
Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Misri jana tarehe 28 Safar walishiriki katika majlisi za maombolezo ya kukumbuka siku ya kuaga dunia Mtume Muhammad (saw) katika Msikiti wa Imam Hussein (as) mjini Cairo.
Vikao na majlisi kama hizo za maombolezo ya kukumbuka tukio chungu za kuaga duniani Mtukufu Mtume (saw) pia zimefanyika katika nyumba mbalimbali za Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Misri.
Sayyid Taha al Hashimi mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as) alihutubia majlisi ya Msikiti wa Imam Hussein mjini Cairo akizungumzia sifa za kipekee za Nabii Muhammad (saw) na kusisistiza kuwa vikao na majlisi kama hizo zinazohudhuriwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia na wapenzi wa Ahlul Bait (as) ni jibu bora kwa watu wanaotaka kuchafua sura safi na Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu kwa mambo ya uzushi na hurafa.
Maulamaa na wasomi waliohutubia majlisi hizo wamesisitiza juu ya umoja na mshikamano baina ya Waislamu wote, udharura wa kujiepusha na mifarakano na kushikamana na Mtume Muhammad ambaye ndiye nguzo ya umma wa Kiislamu.
Sehemu nyingine ya majlisi hizo ilihusu kiraa ya Qur'ani Tukufu na dua za kuitakia heri Misri, wananchi na mapinduzi yao. 939647

captcha