Kongamano hilo litachunguza sira na maisha ya Prf. Muhammad Abdullah Qadari, hafidhi kipofu wa Pakistan kama msomi anayefanya bidii kubwa wa Qur'ani.
Prf. Qadari ambaye alizaliwa akiwa kipofu aliweza kuhifadhi Qur'ani nzima kwa kufanya juhudi kubwa na kupata shahada ya uzamivu katika taaluma ya siasa.
Mbali na Qur'ani Tukufu Muhammad Qadari amehifadhi vitabu 200 vikiwemo vya Plato, Aristotle, vitabu vya lugha ya Kiarabu na kadhalika.
Vilevile anazungumza lugha kadhaa zikiwemo za Kiarabu, Kiingereza na Kifarsi. 939660