Kwa mujibu wa tovuti ya Sufiuniversity, mafunzo hayo yataanza tarehe 15 Februari hadi Mei 3.
Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Qur’an Tukufu, risara ya
upendo ya Mwenyezi Mungu, utambuzi wa aya zinazotoa tiba za Qur’ani, njia za kutumia Qur’ani
Tukufu, maarifa ya kina ya Qur’ani, utakatifu wa Qur’ani, chakula cha kiroho cha Qur’ani na kadhalika.
Baada ya kukamilisha mafunzo hayo, wahitimu wanaweza kushiriki katika duru ya pili ya mafunzo ya siri za Qur’ani Tukufu katika chuo hicho. 940723