IQNA

Mafunzo ya Qur’ani kwa waliosilimu katika jeshi la Brunei

16:24 - January 28, 2012
Habari ID: 2262897
Mafunzo maalumu ya Ta’alumul Qur’ani kwa waliosilimu katika Jeshi la Kifalme la Brunei yatamalizika Jumapili 29 Januari.
Kwa mujibu wa tovuti ya asiaone, watu 35 walioikumbatia dini tukufu ya Kiislamu hivi karibuni wanashiriki katika mpango huo.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Kituo cha Kidini cha Jeshi la Kifalme la Brunei kwa lengo la kutoa mafunzo ya kimsingi ya kusoma Qur’ani kwa waliosilimu.
Mpango huo wa Ta’alimul Qur’ani ni sehemu ya mipango ya jeshi la Brunei ya kuimarisha elimu ya Qur’ani miongoni mwa wanajeshi wote nchini humo. Mbali na kujifunza Qur’ani wanajeshi wa Brunei pia wanapata mafunzo ya tadhkira, hadith na sala.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo afisa mwandamizi wa jeshi la Brunei Luteni Kanali Abdul Ghani Haj Abdullah amewaambia washiriki kuwa Qur’ani si kitabu cha kusomwa tu bali ni muongozo wa maisha. Amesema kujifunza Qur’ani bila kutekeleza mafundisho yake hakuna maana.
940635
captcha