IQNA

Mafunzo ya elimu ya kiraa ya Qur'ani yaanza Mauritania

16:49 - January 28, 2012
Habari ID: 2263526
Masomo ya elimu ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yalianza jana katika mji mkuu wa Mauritania, Nouachott.
Mafunzo hayo yatakayoendelea kwa kipindi cha miezi mitatu kwa hima ya Jumuiya ya Kiislamu ya Wasimamizi wa Misikiti, yanawashirikisha watu 60 wakiwemo wavulana na wasichana wanaovutiwa na kiraa ya Qur'ani.
Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Wasimamizi wa Misikiti nchini Mauritania Muhammad Ould Muhammad ameashiria umuhimu wa tajwidi na kiraa ya Qur'ani Tukufu na kusema kuwa mwishoni mwa masomo hayo kutafanyika mtihani na washindishi watatunukiwa zaidi.
Ameongeza kuwa Jumuiya ya Kiislamu ya Wasimamizi wa Misikiti Mauritania ina nia ya kutoa mafunzo ya hadithi, fiqhi ya Kiislamu na usulu na kueneza elimu na maarifa ya Kiislamu kwa njia hiyo. 941988

captcha