IQNA

Wabahrain wakusanya nakala milioni moja za Qur'ani kwa ajili ya Afrika

17:51 - January 28, 2012
Habari ID: 2263537
Mpango wa kukusanya nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu kwa ajili ya bara la Afrika umeanza kutekelezwa nchini Bahrain kwa hima ya Jumuiya ya Vyombo vya Habari vya nchi hiyo.
Shirika la Habari la Bahrain BNA limeripoti kuwa nakala hizo milioni moja za Qur'ani Tukufu zitatumwa barani Afrika chini ya mpango wa 'Nakala Milioni Moja za Qur'ani Tukufu, Zawadi ya Bahrain kwa Afrika'.
Mpango huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa wananchi wa Bahrain, jumuiya za ndani na nje ya nchi. Maulamaa wa Bahrain wamekaribisha mpango huo wa kukusanya nakala milioni moja za Qur'ani kwa ajili ya Afrika.
Sheikh Faisal al Gharir amesema Waislamu wa bara la Afrika wanahitajia nakala za Qur'ani Tukufu na kwamba nakala za kitabu hicho ambazo zinapatikana kwa wingi nchini Bahrain si rahisi kupatikana katika maeneo mbalimbali duniani.
Sheikh Issa al Mutawwaa wa Bahrain pia amekaribisha mpango huo na kutoa wito wa kutarjumiwa Qur'ani Tukufu kwa lugha mbalimbali kwa lengo la kueneza zaidi mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu. 941758

captcha