IQNA

Semina ya muujiza wa kielimu wa Qur'ani yafanyika Jordan

16:20 - January 29, 2012
Habari ID: 2264306
Semina inayojadili muujiza wa kielimu wa Qur'ani Tukufu iliyofanyika chini ya anwani ya 'Damu iliyoko kwenye Mishipa ya Mwanadamu ni Dalili ya Kuwepo Mwenyezi Mungu' ilifanyika jana Jumamosi tarehe 28 nchini Jordan.
Semina hiyo ilifanyika kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Wahandisi ya Jordan na Jumuiya ya Muujiza wa Qur'ani ya nch hiyo. Kundi la watafiti wa maudhui ya muujiza wa Qur'ani na wasomi wengine wanaovutiwa na maudhui hiyo walishiriki kwenye semina hiyo.
Akizungumza katika semina hiyo, Abdul Rahman al-Hasou mmoja wa watifiti hao aliwabainishia washiriki jinsi damu inavyozunguka katika mwili wa mwanadamu, kazi ya ubongo na mishipa ya damu, shinikizo la damu, nafasi ya hewa ya oksijeni kwenye damu pamoja na vilevile nafasi ya moyo kwenye maisha ya mwanadamu.
Amefafanua pia nafasi ya seli za damu katika mzunguko wa damu hiyo kwenye mwili wa mwanadamu na kusema kuwa jambo hilo linabainisha wazi muujiza mkubwa wa Mwenyezi Mungu katika kumuumba mwanadamu.
Amezungumzia pia jinsi damu ya mwanadamu inavyosafishwa kwenye figo ya mwanadamu na kusisitiza kwamba jambo hilo hutimia kwa umakini mkubwa. 942375
captcha