IQNA

Msahafu wa kitaifa wa Imarati wachapishwa upya

12:17 - January 31, 2012
Habari ID: 2265513
Msahafu wa kitaifa wa Imarati umechapishwa upya katika mwaka huu wa 1433 Hijiria kwa udhamini wa Idara Kuu ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo WAM, kwa chapa hiyo mpya, Msahafu huo utakuwa umechapishwa kwa mara ya nne mfululizo, ambapo mara hii nuskha laki moja zinatazamiwa kuchapishwa na kuuzwa sokoni.
Muhammad al-Ka'bi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu ya Imarati amesema kwamba Qur'ani hiyo ya kitaifa imechapishwa upya kwa lengo la kusambazwa misikitini na kuchukua nafasi ya nakala za Qur'ani zilizochakaa katika maeneo hayo ya ibada.
Amesema Qur'ani hizo zitatawanywa katika misikiti 5000 ya Imarati. Ameendelea kusema kuwa Qur'ani hizo zilizochapishwa kwa maandishi madogo na makubwa zitawawezesha watu walio na umri tofauti na vilevile walio na matatizo ya macho kuzisoma kirahisi. 943522
captcha