IQNA

Qur'ani ya bao yaonyeshwa kwenye kikao cha mabunge ya Kiislamu

17:02 - February 01, 2012
Habari ID: 2266777
Qur'ani iliyoandikwa kwenye bao ilionyeshwa siku ya Jumatatu pambizoni mwa kikao cha saba cha Baraza Kuu la Muungano wa Mabunge ya Kiislamu katika mji wa Palampang, Indonesia.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Bayan linalochapishwa Imarati, Qur'ani hiyo ya bao ilionyeshwa na Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia ambapo Marzouqi Ali, Spika wa Bunge la Indonesia na wajumbe wengine walioshiriki katika kikao hicho walihudhuria.
Akizungumza katika hafla ya maonyesho ya Qur'ani hiyo, Spika Marzouqi Ali alizungumzia umuhimu wa Qur'ani katika jamii ya Kiislamu na kusema kuwa Qur'ani hiyo iliyoandikwa na kuratibiwa kwa muda wa miaka mitano ilikamilika mwaka 2008. Amesema Qur'ani hiyo iliyoandikwa na kundi la wasanii mashuhuri wa Kiislamu inahifadhiwa katika msikiti mkuu wa Palampang.
Spika Marzouqi Ali ameashiria pia udharura wa kufanyika vikao vya Muungano wa Kiislamu na kusisitiza kuwa vikao hivyo vina nafasi muhimu katika kuimarisha umoja wa nchi za Kiislamu.
Kikao cha saba cha Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiislamu kilimalizika jana Jumanne huko Palampang. 944435
captcha