Sayyid Hamad bin Abdallah al-Mihna, Naibu Mkuu wa Idara ya Tablighi na Mwongozo wa Kidini inayofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar amesema kwamba kuimarishwa uwezo wa mahafidh wa Qur'ani katika vituo vya Qur'ani vya Qatar na vilevile kunyanyuliwa kiwango cha usomaji sahihi wa kitabu hicho kitakatifu cha mbinguni ni miongoni mwa malengo ya kuandaliwa masomo hayo.
Amesema licha ya kuwa watu wanaoshiriki katika masomo hayo kimsingi ni walimu na mahafidh wa Qura'ni, lakini walimu wa masomo mengine ya Kiislamu na vilevile wanachuo wa Qatar wanaweza pia kushiriki.
Masomo hayo yamepangwa kufanyika kwa muda wa siku kumi kati ya swala mbili za Maghrib na Ishaa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya mahafidh na walimu wa Qur'ani 100 wamejiandikisha kushiriki masomo hayo. 945164