Duru ya 12 ya mashindano ya hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa vilema wa viungo vya mwili, yaliyopewa jina la Zawadi ya Ra'sul Kheima yalianza siku ya Jumanne katika ufalme huo unaounda Umoja wa Falme za Kiarabu.
Washindani 33 wanashiriki katika mashindano hayo yanayotazamiwa kukamilika rasmi hii leo Alkhamisi. Mashindano hayo yanasimamiwa na wanachama wa Sekretarieti ya Mashindano na Taasisi za Qur'ani Tukufu ya Ra'sul Kheima.
Ilham bint Abdul Aziz bin Hamid al-Qasimi, mkuu wa Kituo cha Malezi na Uwezeshaji wa Vilema cha Ra'sul Kheima ambaye pia anashirikiana na waandaji wa mashindano hayo katika kuyafanikisha ametoa hotuba muhimu ya ufunguzi. Amesema lengo kuu la kuandaliwa mashindano kama hayo ni kulea na kuwahudumia vilema katika jamii ya Qatar.
Al-Qasimi ameongeza kuwa kunyanyua viwango vya hifdhi na usomaji Qur'ani, huduma, vipawa na uzoefu wa vilema ni miongoni mwa malengo muhimu yanayofuatiliwa na taasisi za masomo ya Qur'ani za Ra'sul Kheima. 945165