IQNA

Olimpiadi ya Qur'ani ya wanachuo wa kigeni Iran kuanza kesho

14:27 - February 04, 2012
Habari ID: 2267717
Awamu ya mwisho ya Olimpiadi ya 17 ya Qur'ani na Hadithi kwa ajli ya wanachuo wa kigeni nchini Iran katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa itaanza kesho Februari 5.
Akizungumza na IQNA, mkuu wa idara ya Olimpiadi hiyo Bw. Alireza Qorbani amesema mashindano hayo yataanza kwa qiraa ya qari aliyeshinda katika mashindano yaliyopita na kuendelea kwa hotuba ya Bw. Hussein Asadi Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Qur'ani na Hadithi katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Fiqhi wa Ahul Bayt AS. Amesema anwani ya siku ya kwanza ya mashindano hayo ni ' Qur'ani, Mapinduzi ya Kiislamu, Basirah na Mwamko wa Kiislamu'.
Qorbani amesema kuwa 'Qur'ani, Uongozi wa Kiislamu na Imam Khomeini' ndio anwani ya siku ya pili ya mashindano hayo katika kitengo cha wanaume.
Wanachuo wa kike watashindana katika siku ya tatu ambapo anwani ya siku hiyo itakuwa, 'Qur'ani, Maadili, Malezi na Familia ya Kiislamu'.
Siku ya mwisho ya olimpiadi hiyo yaani, Februari 9, anwani yake itakuwa ni 'Qur'ani, Mtume Mtukufu SAW na Ahlul Bayt AS'.
Imearifiwa kuwa wanaharakati 120 wa Qur'ani watashiriki katika fainali ya olimpiadi hiyo ambapo 83 ni wanachuo wa kigeni wanaosoma Iran na 37 wanasoma katika nchi za kigeni.
944980
captcha