IQNA

Waislamu Ufaransa watakiwa kuadhimisha Miladun Nabi

14:41 - February 04, 2012
Habari ID: 2267934
Baraza Kuu la Waislamu Ufaransa (CFCM) limetoa wito kwa Waislamu nchini humo kuandaa sherehe adhimu kwa mnasaba wa Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW.
Baraza hilo limetoa taarifa na kutangaza Jumamosi Februari Nne kuwa Siku Kuu ya Maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Mtukufu wa Uislamu Muhammad Al Mustafa SAW.
Taarifa hiyo imewataka Waislamu wote Ufaransa kushiriki katika hafla za kidini kwa mnasaba huu adhimu na kutumia fursa hii kuutangaza Uislamu.
Taarifa hiyo imesema: 'Sherehe za Maulidi ya Mtume SAW ni fursa kwa Waislamu kumuarifisha Mtume wa amani na rehma kwa wasio kuwa Waislamu na kufungua njia ya mazungumzo na wafuasi wa dini zingine.
Baraza Kuu la Waislamu Ufaransa pia limewapongeza Waislamu wote wa Ufaransa kwa mnasaba wa siku uu adhimu ya Miladun Nabi na kuelezea matumaini kuwa sherehe hizi zitakuwa fursa ya kuutangaza Uislamu halisi duniani.
946106
captcha