IQNA

Juzuu ya mwisho ya Qur'ani yatarjumiwa kwa lugha nne za Kiafrika

11:20 - February 05, 2012
Habari ID: 2268661
Juzuu ya 30 ambayo ni juzuu ya mwisho ya Qur'ani Tukufu imetajumiwa kwa lugha nne za Kiafrika kwa udhamini wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamduni wa Kiislamu ISESCO.
Kwa mujibu wa gazeti la Yaum as-Sabi' la nchini Misri, tarjumi ya juzuu hiyo ni miongoni mwa vitabu vinavyochapishwa na kusambazwa na shirika hilo kwa ligha nne za Kiafrika za Ulof, Sanghai, Mandingo na Luganda.
Isesco imesema kwamba imeshirikiana na Chuo ha Kimataifa cha Africa nchini Sudan kwa lengo la kutarjumu vitabu vya kiutamaduni na Kiislamu kwa lugha nne zilizotajwa za Kiafrika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, awali shirika hilo lilitarjumu juzuu hiyo ya 30 katika lugha nyingine za Kiafrika za Kihausa, Kifulani, Kisomali, Kiswahili na Kiyoruba. 946798
captcha