Kile ambacho kinajiri katika Ulimwengu wa Kiislamu leo, kutoka vita na fitina za kimadhehebu huko Iraq hadi kadhia ya Syria na vitisho dhidi ya Iran, yote hayo ni kati ya njama za Wazayuni za kuibua migogoro na kupotosha fikra za walimwengu kutoka mpango hatari unaoendelea wa Kuyahudisha Quds Tukufu.
Haya ni kwa mujibu wa mwanachama wa Harakati ya Kisiasa ya Amal ya Lebanon Hassan Qabalan. Akizungumza na IQNA amesema tokea vita vya mwaka 1976 kati ya nchi za Kiarabu na Utawala wa Kizayuni, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuyahudisha Quds Tukufu ni njama ambazo zimekuwa zikiendelea kwa kasi.
'Wazayuni wanalenga utambulisho wa Kiarabu na Kiislamu wa Quds Tukufu', amesisitiza.
Amesema Quds si mji wa kawaida kwani ni kibla cha kwanza cha Waislamu na sehemu ya tatu kwa utakatifu katika Uislamu.
Qabalan ameonya kuwa Wazayuni wakiruhusiwa kuyahudisha Quds Tukufu basi huo utakuwa mwanzo wa njama za kuangamiza mataifa mengine ya Kiislamu.
Qabalan amesema kushindwa Waislamu kukabiliana na changamoto hii ya Wazayuni kunatokana na kujishughulisha na hitilafu za kimadhehebu, jambo ambalo limewapa Wazayuni fursa ya kuendeleza njama zao za kishetani za kuyahudisha Quds Tukufu.
Amekosoa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kwa kushinda kutetea na kuuhami mji wa Quds. Mwanharakati huyo wa Lebanon amesisiza kuwa kadhia ya Quds na Palestina haiwezi kutatuliwa kupitia mazungumzo.
945815