IQNA

Maadhimisho ya mwaka wa 225 tokea ichapishwa Qura'ani kwa Kirusi

15:57 - February 05, 2012
Habari ID: 2268758
Waislamu nchini Russia hasa katika jimbo la Tatarstan wanapanga kuadhimisha 'Mwaka wa Qur'ani' mwaka huu wa 2012 kwa mnasaba wa mwaka wa 225 tokea ichapishwe Qur'ani ya kwanza iliyotarjumiwa kwa Kirusi.
Qur'ani hii ilitarjumiwa mwaka 1787 kwa amri ya Malkia Ekaterina II kwa mujibu wa tarjumi ya wanazuoni wa Tatarstan.
Nuskha hii baadaye ilitumiwa kama kigezo cha misahafu yote ya lugha ya Kirusi ambayo inatumiwa na Waislamu wa Russia.
Kuna Qur'ani 600 zilizotarjumiwa kwa lugha mbalimbali katika Jumba la Makumbusho la Kiislamu katika eneo la Kazan Kremlin nchini Russia.
'Mwaka wa Qur'ani Tatarstan utawawezesha wakazi wa eneo hilo kufahamu mafundisho ya Qur'ani, amesema Ildus Xazra Faizvo Mufti wa Tatarstan.
Jamhuri ya Tatarstan ambayo mji wake mkuu ni Kazan ni sehemu ya Shirikisho la Russia na iko katika Jimbo la Volga.
947495
captcha