IQNA

Wito wa kuundwa Muungano wa Kiislamu Algeria

16:06 - February 05, 2012
Habari ID: 2268764
Chama cha Marekebisho ya Kitaifa Algeria kimetoa wito kwa vyama vyote vya Kiislamu nchini humo kuunda Muungano wa Kiislamu utakaoshiriki katika uchaguzi ujao wa bunge.
Kwa mujibu wa tovuti ya elwatan, Hamlawi Akushi Katibu Mkuu wa Chama cha Marekebisho ya Kitaifa amesisitiza kuwa kutoungana vyama vya Kiislamu katika uchaguzi ujao wa bunge kutapelekea vyama hivyo kushindwa. Amesema, 'vyama vya Kiislamu lazima viunde muungano mkubwa ili viweze kupata ushindi mutlaki katika uchaguzi wa bunge'.
Ameendelea kuwa kuundwa muungano wa vyama vya Kiislamu ni jambo ambalo pia linaweza kuzuia aina yoyote ya wizi wa kura katika uchaguzi. Amesema chama chake kiko tayari kukumbatia chama chochote cha Kiislamu kwa lengo la umoja.
Itakumbukwa kuwa katika miaka ya hivi karibuni vyama vya Kiislamu Algeria vimekuwa vikipata kura nyingi lakini kutokana na kuwa havina umoja havijaweza kuunda serikali.
947411
captcha