IQNA

Tarjumi mpya ya Qur'ani kwa lugha ya Kichina yazinduliwa

16:14 - February 05, 2012
Habari ID: 2268989
Sherehe za kuonyeshwa tarjumi mpya ya Qur'ani kwa lugha ya Kichina ilifanyika jana katika Jumuiya ya Wakfu na Masuala ya Kheri nchini Iran.
Sherehe hiyo imefanyika sambamba na maadhimisho yanayofanyika kote nchini ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Sherehe hiyo imehudhuriwa na mtarjumi wa Qur'ani hiyo, mwakilishi wa Faqihi Mtawala, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakfu ya Masuala ya Kheri na viongozi kadhaa wa taasisi mbalimbali.
Tarjumi hiyo imendikwa na Sulaiman Bajiso ambaye ni Mchina aliyehitimu sayansi za kidini nchini Iran na ametumia miaka kumi kukamilisha tarjumi hiyo. 946963


captcha