IQNA

Mtarjumi wa kwanza wa Qur'ani kwa lugha ya Kikurdi afariki dunia

15:58 - February 05, 2012
Habari ID: 2268990
Mtarjumi wa kwanza wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kikurdi nchini Uturuki Mulla Abdullah Farly alifariki dunia jana katika hospitali ya Bin Sina katika mji wa Aghry nchini Uturuki akiwa na umri wa miaka 72.
Tovuti ya Turkia al Youm imeripoti kuwa Mulla Abdullah Farly alikuwa mtu wa kwanza aliyetarjumu tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kikurdi hapo mwaka 1997.
Mulla Abdullah Farly alikuwa miongoni mwa wanaharakati wa masuala ya Qur'ani wa Uturuki na alifanya uhakiki mkubwa kuhusu mshairi na mwanafasihi mashuhuri wa Kikurdi Ahmad Khani.
Mwili wa mwanaharakati huyo wa masuala ya Qur'ani ulizikwa jana katika mji alikozaliwa wa Van huko mashariki mwa Uturuki. 947603


captcha