IQNA

Duru ya 13 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani yafanyika Imarati

11:55 - February 06, 2012
Habari ID: 2269439
Duru ya 13 ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu Zawadi ya Dubai yanaendelea kufanyika nchini Imarati kwa kuwashirikisha washindani kutoka kila pembe ya umoja huo wa Kiarabu.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Bayan la nchi hiyo, mashindano hayo yaliyoanza siku ya Jumamosi Februari Nne kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw) yanatazamiwa kumalizika Jumamosi tarehe 11 Februari.
Wanawake wanaoshiriki mashindano hayo wanashindana katika eneo la al-Humeira katika mji wa Dubai na wanaume katika eneo la al-Quseis katika mji huohuo.
Washindani 296 walishiriki katika mashindano hayo mwaka uliopita ambapo mwaka huu washindani hao ni 302.
Washindani wanachuana kuhifadhi kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika makundi tofauti ya hifdhi ya kitabu kizima, hifdhi ya juzuu 20, juzuu 10, juzuu 5 na juzuu tatu za kitabu hicho cha mbinguni. 948178
captcha