IQNA

Mashindano ya 12 ya Kimataifa ya Qur'ani yafanyika Russia

16:25 - February 06, 2012
Habari ID: 2269821
Duru ya 12 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Russia ilifanyika jana katika mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.
Mashindano hayo yamefanyika kwa hima ya Baraza la Mamufti wa Russia kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhisha Qur'ani. Mashindano hayo yamewashirikisha maqari 38 katika uwanja wa hifdhi ya Qur'ani nzima.
Kamati ya majaji wa mashindano hayo ilikuwa na watu watano akiwemo Imad Zuhair Hafidh.
Mufti Mkuu wa Russia Ravil Gainutdin alihutubia sherehe za kufunga mashindano hayo na kuzishukuru jumuiya na watu wote waliofanikisha mashindano hayo.
Sherehe za kufunga mashindano hayo na kuwatunza washiriki zimehudhuriwa na mabalozi wa nchi za kigeni, maulama, wanafikra na wanaharakati wa masuala ya Qur'ani. 948216


captcha