Taarifa ya Hamas imebainisha kwamba, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni una lengo la kuuyahuidisha mji huo na kutokomeza kabisa utambulisho wa Kiislamu na Kikristo katika eneo hilo.
Chama cha Hamas kimesisitiza kwamba, hatua hiyo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na wakati huo huo ni kudharua matukufu ya dini za mbinguni.
Hamas imeutaka Umoja wa Mataifa na asasi za haki za binadamu ulimwenguni kuchukua hatua za kusitisha mipango michafu ya Wazayuni maghasibu huko Quds.
Aidha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuutaka ukomeshe vitendo na hatua zake za kinyama za kupora ardhi za wananchi wa Palestina.
948209